Mwili wa aliyekuwa Katibu katika wilaya ya Songea Ndugu Josephat Ndulango leo hii umeagwa rasmi katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Ndugu Ndulango alifikwa na umauti juzi baada ya kuugua kwa kipindi kirefu
Mh. Mboni Mhita akipita mbele ya jeneza kuaga mwili wa marehemu Ndulango
Marehemu alikuwa akikitumikia chama cha Mapinduzi CCM katika maisha yake yote na mpaka anakutwa na umauti alikuwa akishika wadhifa wa ukatibu wa wilaya ya Songea
Kutoka kushoto ni Ndugu Halima Bulembo, Katikati ni Mh. Mboni Mhita na kushoto ni Ndugu Sixtus Mapunda wakiwa katika eneo la Hospitali ya Lugalo ulipoagwa mwili wa Marehemu Ndulango
Baadhi ya waheshimiwa waliohudhuria katika kuuaga mwili wa marehemu Ndulango.kutoka kulia ni Ndugu Mfaume Kizigo( Naibu katibu mkuu UVCCM Taifa), Mh. Stevene Wasira (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mh. Mboni Mhita (Makamu mwenyekiti UVCCM Taifa/Naibu katibu mkuu P.Y.U Afrika ya Mashariki)
Dr. Nchimbi na Mh. Ridhiwani Kikwete wakipita mbele ya jeneza la marehemu Josephat Ndulango
Dr. Nchimbi na Mh. Ridhiwani Kikwete wakipita mbele ya jeneza la marehemu Josephat Ndulango
Marehemu Ndulango atazikwakesho huko Ifakara mkoani Morogoro.
Post a Comment