0
Kile kitendaeili cha nani ataibuka mshindi katika mechi ya nani mtani jembe kati ya klabu ya Simba na Yanga kimeteguliwa leo kwa Simba kuibuka kifua mbele kwa kuwabugiza watani wao magoli 2-0
magoli yote yakifungwa katika kipindi cha kwanza, katika mchezo huo Yanga walionekana kuanza mpira kwa kasi kwa kulisakama lango la Simba huku mshambuliaji wao mpya kutoka Liberia Sherman akionekana kuisumbua vilivyo ngome ya Simba. kibao kiliwageukia Yanga mara baada ya Awadhi Juma kuifungia Simba goli la kuongoza kabla ya Maguri kuongeza la pili na la mwisho katika mchezo huo na kuifanya Simba kuendeleza ubabe kwa Yanga kwani katika mchuano kama huo uliofanyika mwaka jana klabu ya Simba ilishinda magoli 3-1..katika mechi ya leo Emanuel Okwi ndio alikua mwiba kwa ngome ya Yanga.
 Awadh Juma na Jonas Mkude wakishangilia goli
Mashabiki wa Simba wakishangilia goli la kwanza
 Cotinho akijaribu kuitoka ngome ya Simba
 Sherman akiwakusanya mabeki wa Simba
 Ni nderemo na vifijo kwa benchi la Simba
Kidedea kikichezwa uwanjani mara baada ya wekundu wa msimbazi kupata goli la kwanza

Post a Comment

 
Top