0

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera, Mbunge wa Morogoro Kusini  Mhe Innocent Kalogeris na Katibu wa Rais Bw. Prosper Mbena wakiongea ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki mkoani Morogoro 

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri zawadi ya picha ya jengo la makao makuu ya TAZARA akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro


 Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri (kulia) na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na umati mkubwa wa watu baada ya kuwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika mkoa wa Morogoro

PICHA NA IKULU

Post a Comment

 
Top